Wenger aliona kama Mourinho amemkosea heshima kwa kumbwatukia na ndipo akaamua kumfuata akitaka kumtandika kofi lakini waliishia kusukumana kama vile wanakumbusha michezo yao ya zamani wakiwa watoto.
Wenger kacharuka! we Mourinho umezoea kuniropokea kama mtoto mdogo, hujua kama mimi ni kakayako?...na unikome kabisa. |
Mchezo wa leo ulikuwa mzuri sana kwa kuwa timu zote zilikuwa zimekamiana, lakini kadiri muda ulivyokuwa unakwenda Chelsea walizidisha mbinu na kufanikiwa kupata goli la kwanza kwa njia ya penati dakika ya 27 kupitia Eden Hazard huku goli la pili likifungwa naye Diego Costa dakika ya 78 baada ya kuwachomoka mabeki wa Arsenal.
0 comments:
Post a Comment