Hiyo ni picha inayo onyesha jinsi Wenger alivyo mfuata Mourinho na kumsukuma katika mechi ya wikiendi iliyo pita ambayo Chelsea iliibuka na ushindi wa Magoli 2-0. Wenger alifanya tukio hilo baada ya kujibizana na Mourinho juu ya rafu aliyo chezewa Alex Sanchez na beki wa Chelsea, Gary Cahill. |
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror na kituo cha televisheni cha Telefoot, Wenger amesema watu wametia sana chumvi katika tukio lililo tokea kati yake na Mourinho wikiendi iliyopita na kuupa uzito mkubwa ambao pengine isinge stahili.
"Watu wamelikuza sana jambo hilo, lakini pia nadhani nisinge paswa kufanya vile nilivofanya kwa kuwa siyo siyo picha nzuri katika mpira.
"Siku zote sipendezwi na hali yoyote ya uhasama na kwa kutambua hilo, naomba msamaha kwa kitendo nilicho kifanya kwa kocha mwenzangu, Mourinho. Hali ya hasira humtokea mtu yeyote. Lakini pia ikumbukwe sikuingia katika eneo la Mourihno kama ambavyo watu wanasema"
Mpaka sasa bado shirikisho la kandanda nchini Uingerza FA, halijasema litachuakua hatua gani dhidi ya Wenger na mwenzake Mourinho.
0 comments:
Post a Comment