DUNIANI kote! watu hujipatia fedha nyingi na kujenga
heshima kubwa ndani na nje ya nchi zao kupitia vipaji walivyojaaliwa na Mungu
muumba.
Watu kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Wayne Rooney,
Yaya Toure, Didier Drogba na wengineo, wana utajiri mkubwa kupitia miguu yao
iliyobarikiwa kutandaza soka.
Hata Tanzania kuna wanasoka wengi wanaovuna mamilioni ya fedha kupitia vipaji vyao.
Mbali na soka, wengine wana vipaji vikubwa vya
muziki , uchekeshaji, maigizo na taaluma mbalimbali.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojaa vijana wengi
wenye vipaji vikubwa katika mambo tofauti tofauti, lakini fursa ya kuonekana
imekuwa adimu sana.
Ni kawaida kabisa kupita mitaani na kuwakuta vijana
wenye uwezo wa kuchekesha na kuigiza, lakini hawana kwa kwenda.
Kwa kulitambua hilo kituo bora cha Azam TV
kimedhamiria kutoa fursa kwa watu wote wanaojihisi wana vipaji vya uchekeshaji,
lakini hawajapata nafasi ya kuonekana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Katika kuhakikisa hilo, Azam TV imeandaa kipindi cha
ucheshi cha Luninga kiitwacho WASAKATONGE COMEDY SHOW na usahili kwa ajili ya
kutafuta wenye vipaji vya kuchekesha jukwaani na kuigiza vichekesho unatarajia
kufanyika ijumaa ya Oktoba 10, 2014, kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni ndani ya uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Usahili huo utajali misingi ya haki na mwenye uwezo
pekee ndiye atakayepata nafasi ya kusonga mbele, hivyo kila mtu afike kujaribu
bahati yake.
Mchakato huu utaegemea zaidi katika kigezo cha
Ubunifu kwa minajili ya kuchekesha, kuwa mwepesi katika ucheshi, kuwa na mawazo
ya haraka katika ucheshi na jinsi gani anaweza kushirikiana na wenzako kama
timu moja.
Kwa mshiriki yeyote
yule kutoka nje ya mkoa wa Dar es salaam bado ana nafasi ya kushiriki usahili
isipokuwa gharama zote zitakuwa juu yake.
Ili kutengeneza timu ya WASAKATONGE mchakato utakuwa
wa awamu mbili;-
Mosi; kutakuwa
na usahili wa wazi utakaofanyika uwanja wa ndani wa taifa (Indoor); kwa wale
wachache watakaopita kulingana na hitaji la kamati watapewa utaratibu juu ya
kipi kitakachoendelea kwa mzunguko wa pili.
Pili; kutakuwa na mchujo utakaopelekea kuchaguliwa
kwa watu wachache, wasiozidi kumi na hao ndio watakaotengenezwa kwa kupatiwa
mafunzo ili kuwa wachekeshaji/waigizaji. Watakaobahatika watakuwa WASAKATONGE wa Azam tv.
Mambo ya Zingatia!!!
Usaili huu ni wa wazi, Wasahiliwa watapaswa
kujigharamia usafiri na chakula, Hakuna zawadi kwa washindi. Mafunzo ya
uchekeshaji yatatolewa kwa washindi 10
WASAKATONGE, Ni zaidi ya COMEDY
0 comments:
Post a Comment