Monday, October 13, 2014


Dk. Damas Ndumbaro


Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania, TFF limemfungia Dr.Damas Ndumbaro kuto jihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nje ya nchi ya Tanzaina kwa muda wa miaka saba kwa sababu mbalimbali mojawapo ikiwa ni kupotosha klabu za ligi kuu  kuhusu makato ya asiliamia tano iliyotangazwa  na TFF hivi karibuni.

Baada ya TFF kutangaza makato hayo klabu nyingi za ligi kuu kupitia mwanasheria wao Damas Ndumbaro zilikataa kwa kishindo suala hilo huku zikitishia kugomea ligi endapo TFF itapitisha makato hayo kwa nguvu. Makato ya asiliamia tano ambayo TFF imetaka klabu zilipe zilikuwa zinatokana na wadhamini wa ligi ambao ni Vodacom na Azam TV.

Makato hayo yalikuwa yakilenga kusaidia soka la vijana wadogo ambao ndilo linaaminika kuwa njia sahihi ya kupata wachezaji bora kwa ajili ya kusaidia nchi yetu kisoka.

Inaaminika kwamba Ndumbaro alikuwa akipindisha baadhi ya vipengele vilivyopo katika katiba ya bodi ya ligi ya tanzania ili kuwatetea wateja wake(klabu) wasikubaliane na suala hilo, kitu ambacho ni kosa kisheria kufanya hivyo.

Dk. Damas Ndumbaro  ni mjumbe wa bodi ya ligi na mwanasheria wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video