Wednesday, October 15, 2014



KOCHA wa timu ya Taifa ya Sudan,  Abdallah Mohammed Mazda amesema mechi ya leo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON 2015 nchini Morocco dhidi ya Nigeria anaipa uzito wa hali juu na anaamini timu hiyo inaweza kufanya vizuri mara mbili mbele ya Super Eagles.
Mazda baada ya mazoezi ya timu yake jana nchini Nigeria, alisema vijana wake wanaweza kuwawashia moto wenyeji kwa mara nyingine na kuibuka na pointi tatu.
"Nawaheshimu sana Nigeria. Kiukweli naipenda timu hii. Kocha (Stephen) Keshi ni rafiki yangu, lakini huo ndio mpira. Tunafanya kazi uwanjani," alisema kocha huyo.
"Ni uwanja mzuri sana. Hii ni Nigeria, taifa la kiwango cha juu Afrika.
"Nimevutiwa sana na mazingira, nadhani itakuwa mechi nzuri kwa mashabiki wa pande zote".
Mazda anahisi ushindi wa 1-0 waliopata mechi iliyopita dhidi ya Nigeria hauwezi kujirudia kirahisi, lakini wataingia uwanjani kupambana kufa na kupona kwasababu wana nafasi ya kucheza fainali hizo mwezi januari.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video