Na Frank Momanyi Mgunga, Dar es salaam
WAKATI timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars
ikitarajiwa kushuka ugani hapo kesho katika mtanange wa kukata na shoka dhidi
ya timu ya taifa ya Benin mchezo utakaopigwa katika dimba la uwanja wa taifa
jijini Dar es salaam, baadhi ya wadau wa soka nchini wamesema wana imani na timu
hiyo kuwa itapeperusha vyema bendera ya
Tanzania katika mchezo wa hapo kesho.
Akiongea na MPENJA BLOG, mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga Seklojo Chambua
amesema mchezo wa hapo kesho ni kiwango sahihi kwa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro premium lager chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij ambaye anapenda
kutumia mfumo wa 4-3-3, lakini je mfumo huo utaweza kuizamisha Benin ?
Chambua alisema mfumo wa kocha sio kigezo cha
kuifanya timu yoyote kuweza kuibuka na ushindi bali juhudi binafsi za wachezaji
zinaweza kuipa ushindi timu yoyote ile duniani.
‘’Mfumo wa kocha sio kigezo cha kuifanya timu
yoyote kuweza kuibuka na ushindi bali
juhudi binafsi za wachezaji na ushirikiano ndio unaweza kuipa ushindi timu yoyote ile duniani, kwa
hiyo wachezaji wanatakiwa kujituma hapo kesho ili kuhakikisha wanaipa ushindi
Taifa”. Alisema Chambua.
Kwa upande mwingine Chambua alisema wingi wa
mashabiki katika mchezo wa kesho itakuwa
ni chachu kwa timu ya taifa kuweza kuibuka na ushindi.
Stars ambayo inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kipigo kutoka kwa timu ya taifa
ya Msumbiji na kuweza kuondolewa katika mitanange ya kufuzu michuano ya kombe
la mataifa barani Afrika, hapo kesho itashuka ugani ikiwategemea wachezaji wake
mahili wanaocheza soka la kulipwa , Thomas ulimwengu, Mwinyi Kazimoto pamoja na
Juma Luizio anayekipiga katika klabu ya Zesco fc ya nchini Zambia.
0 comments:
Post a Comment