HOFU imeanza kupungua katika klabu ya Simba SC
kufuatia kipa namba moja wa klabu hiyo, Ivo Philip Mapunda kuanza mazoezi mjini
Johannesburg nchini Afrika kusini ambako klabu hiyo imewaka kambi kujiwinda na
mechi ya watani wa jadi dhidi ya Yanga itayopigwa Oktoba 18 mwaka huu uwanja wa
TaifA, Dar es salaam.
Ivo aliyeumia kidole katika mazoezi ya Simba zaidi
ya wiki mbili zilizopita mjini Zanzibar alioneka kuwa fiti, hivyo kuwatia moyo
wachezaji wenzake.
Joto lilizidi kupanda Msimbazi kufuatia kipa aliyetegemewa
kucheza mechi hiyo, Hussein Sharrif ‘Casillas’ kuumia ugoko na katika mazoezi
ya jana hakushiriki kabisa.
Kurejea kwa Ivo kutaliweka lango la Simba katika
mikono salama kwasababu Peter Manyika asingeweza kuhimili presha ya mechi hiyo.
Kabla ya kwenda Bondeni, Ivo aliuambia mtandao huu
kuwa Simba inazidi kuiamarika na wana matumaini ya kufanya vizuri mechi zijazo
kuanzia ya Yanga.
“Mashabiki wasife moyo, tulianza kwa sare tatu.
Mengi yanazungumzwa, lakini hakuna haja ya kushikana uchawi, kikubwa ni
kujiandaa na tunaamini tutaweza kufanya vizuri”. Alisema Ivo.
Aidha, aliongeza kuwa kama Casillas atasimama
langoni haitakuwa na tatizo kwasababu ni kipa mzuri, lakini atahitaji kujiamini
zaidi kwasababu hajawahi kucheza kwenye mechi ya presha kama hiyo.
Simba ipo kambini nchini Afrika kusini na
inatarajia kurejea siku moja kabla ya mechi ya jumamosi.
0 comments:
Post a Comment