Sturridge akipokea maelekezo fulani kutoka kwa kocha wake, Brendan Rodgers katika moja ya mechi za ligi kuu nchini Uingereza 2014/2015 |
Tangu Sept 3, 2014, mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge amekuwa nje ya dimba kwa sababu ya maumivu ya misuli ya paja (thigh injury) yaliyokuwa yakimsumbua ambayo aliyapata wakati akichezea timu yake ya taifa ya Uingereza dhidi ya Norway, mchezo ambao ulimalizika kwa Uingereza kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Baada ya kukaa nje ya dimba kwa takribani wiki mbili akiuguza jeraha lake hilo, hivi karibuni Sturridge alirudi uwanjani kuungana na wachezaji wenzake wa Liverpool katika kambi ya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo migine ya ligi kuu ambapo alipata jeraha ligine la misuli ya mguu (calf injury).
"Tulikuwa tunategemea Daniel Sturridge atarudi uwanjani kuanzia Jumapili Oct 19, 2014 wakati tukicheza dhidi ya Queens Park Rangers, lakini sidhani kama tutakuwa naye kwa sababu tayari anasumbuliwa na misuli ya miguu kwa mara nyingine tena," Hiyo ni kauli yake kocha wa Liverpool Brendan Rodgers akizungumza na waaandisha wa habari jana.
Taarifa zinasema kwamba Daniel Sturridge atakuwa nje ya uwanja kwa muda mwezi mmoja akiuguza majeraha yake hayo.
0 comments:
Post a Comment