Usiku wa jana Oct 9, 2014 ulikuwa ni usiku mzuri sana kwa timu ya taifa ya Uingereza katika dimba la kimataifa la Wembley, baada ya kuweza kutoka na ushindi mnene wa magoi 5-0 dhidi ya San Marino.
Kulia ni Roy Hogson, akiwa na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Man U, Wayne Mark Rooney wakizungumza na waandishi wa habari.
|
"Tulikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga magoli mengi zaidi ya hayo matano tuliyofunga kwani kadiri muda ulivyokuwa una kwenda, wachezaji wangu walikuwa wakiongezeka morali ya kutaka kuongeza magoli mengine.
"Angalia jinsi wachezaji wangu walivyokuwa wakimiliki mpira kwa muda mrefu huku waki chachafya goli la wapinzani; naweza kusema hatukuwa na bahati zaidi ya hapo lakini yote kwa yote nawshukuru sana vijana wangu kwa kazi nzuri waliyo ifanya." Hiyo ni kauli ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hogson.
Wafungaji wa Uingereza (Three lions) ni Phil Jagielka, Wayne Rooney (magoli 2), Danny Welbeck, Andros townsend.
0 comments:
Post a Comment