Raheem Sterling amerudi mazoezini katika uwanja wa Liverpool wa Melwood
KIUNGO wa Liverpool, Raheem Sterling amerudi jana mazoenini katika uwanja wa Melwood kufuatia kuzuka utata katika ombi lake la kutoanza kikosi cha England kilichoshinda bao 1-0 dhidi ya Estobia kwasababu ya uchovu.
Sterling alikuwa anafanya mazoezi ya kuongeza kasi na kumiliki mpira katika uwanja wa mazoezi wa Anfield akiwa sambamba na Steven Gerrard, Mario Balotelli na Glen Johnson.
Baada ya mazoezi hayo, nyota huyo mwenye miaka 19 aliondoka na mchezaji mwenzake wa Liverpool na England Jordan Henderson.
Sterling akimiliki mpira katika mazoezi yake ya kwanza tangu arudi kutoka katika majukumu ya kimataifa
0 comments:
Post a Comment