RIP.Senzo Meyiwa. |
Mwenyikiti wa klabu Olando Pirates, Irvin Khoza amesema jezi ya aliyekuwa mlinda lando wa klabu hiyo Senzo Meyiwa amabye aliuwawa usiku wa Jumapili iliyopita, haitavaliwa na mchezaji mwingine yeyote klabuni hapo na badala yake itahifadhiwa kwa ajili ya kumbumbu.
"Sidhani kama kuna mchezaji mwingine atakaeweza kuwa mbadala wa Senzo Meyiwa katika klabu yetu, na wala sidhani kama kuna mtu anatakiwa kuridhi jezi yake (nambari 1). Hiyo jezi haitavaliwa na mchezaji yeyote katika klabu ya Olando Pirates, itabakia kuwa kumbukumbu". Khoza alisema.
Meyiwa 27, ambaye alikuwa ni mchezaji wa Bafabafana na nahodha katika klabu ya Olando Pirates, alipigwa risasi na watu wasiojulikana usiku Jumapili wakati alipokwenda kumtembelea rafiki yake wa kike Ekurhuleni ambaye anaishi katika mji wa Vosloorus nchini Afrika kusini.
Meyiwa anakuwa ni mchezaji wa pili katika klabu ya Olando Pirates kupata heshima ya jezi yake kuhifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu baada ya jezi ya mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Lesley Manyathela kustahafishwa rasmi baada kufa kwa ajali ya gari.
0 comments:
Post a Comment