Kamati ya Utendaji ya Coastal Union imependekeza tarehe ya kufanyika uchaguzi mdogo wa kama ilivyo maagizo ya shirikisho la soka nchini (TFF) kuitaka kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi kwenye safu ya uongozi wa Klabu hiyo.
Kamati hiyo imependekeza kuwa uchaguzi huo utafanyika Novemba 23 mwaka huu mkoani Tanga.
Kauli hiyo imetolewa leo katika kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo barabara kumi jijini Tanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu Mwenyekiti Steven Mguto.
Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siagi amesema kuwa kimsingi uchaguzi huo unafanyika ili kuweza kuziba nafasi zilizokuwa wazi ambayo ni Mwenyekiti na wajumbe wawili wa kamati ya utendaji.
Hata hiyo alisema kuwa wanatarajia kuunda kamati ya uchaguzi ambayo itasimamia uchaguzi huo ili kuweza kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika.
0 comments:
Post a Comment