TIMU ya Taifa ya Nigeria jana ijumaa ilishindwa kufanya mazoezi
katika uwanja wa Khartoum kujiandaa na mechi dhidi ya Sudan kutokana na uwanja
kujaa maji kufuatia mvua kubwa kunyesha Khartoum, mji mkuu wa Sudan.
Super Eagles waliwasili mapema jana na walikuwa na ratiba ya
kufanya mazoezi jioni, lakini ikashindikana kutokana na tatizo hilo.
Msemaji wa timu ya Taifa ya Nigeria, Ben Alaiya baadaye alikiri
kuwa wanatarajia kuripoti suala hilo CAF.
Sudani na Nigeria sitachuana leo jumamosi katika mchezo wa
makundi kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Africa mwakani nchini Morocco.
0 comments:
Post a Comment