Hakuna kitu kizuri katika soka kama ushindi bwana, angalia mshambuliaji nyota wa Bayern Munich , Robert Lewandowski akipokea bonge la busu kutoka kwa MKE wake anayefahamika kwa jina la Anna Sturchuska mbele ya maelfu ya watazamaji waliokuwepo uwanjani Allianz Arena jana, Sep 4, 2014 kushuhudia mtanange wa kukata na shoka kati Bayern dhidi ya Hannover 96 ambapo Bayern waliibuka na ushindi wa magoli 4-0.
|
Ohh baby..!!!! have a kiss please......nice job. Hii ndiyo raha ya ushindi! |
Katika mchezo huo, Lewandoski alifunga magoli mawili na mengine mawili yakafungwa na Muholanzi, Arjen Robben, kitendo kilicho wapoteza kabisa Hannover 96 mchezoni na kujikuta wakiomba mchezo uishe. Kwa mantiki hiyo, Lewandowski sasa anakuwa na jumla ya magoli saba kwa michezo yote aliyocheza ya Bundesliga.
Mpaka sasa Bayern Munich wanaongoza ligi kuu nchini Ujerumani wakiwa na pointi 17 kutoka michezo saba, wanaoburuza mkia ni Werder Bremen ambao wao wamekusanya pointi nne kutoka katika michezo saba
0 comments:
Post a Comment