Ni lazima usalama uwe wa hali ya juu kwa kuwa hata vyombo vilivyopo hapo uwanjani ni vya gharama ya hali ya juu pia |
Ni siku ya pili sasa tangu matajiri wa Dar Azam FC watue pale jijini Mbeya (Green City) tayari kuwakabili wenyeji Mbeya City FC "mapedeshee wa jiji la Mbeya" siku ya Jumamosi Octoba 18, 2014 ikiwa ni mchezo wa nne tangu ligi kuu kuanza Sep 20, 2014.
Ligi kuu Tanzania Bara ilisimama kwa muda wa wiki moja tangu Oct 5, 2014 kupisha mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati yaTaifa Stars ya Tanzania dhidi ya Benin, mchezo ambao ulichezwa Oct 12, 2014 na Stars kutoka kifua mbele uwanjani baada ya kuifumua Benin kwa magoli 4-1 katika dimba la taifa, Dar es salaam.
Kuelekea Jumamosi ya wikiendi ijayo, Oct 18, 2014, timu sita za ligi kuu zitashuka ugani ambapo kati ya mechi zinazotajwa kuwa na ushindani wa hali ya juu siku hiyo ni mchezo wa Simba dhidi ya Yanga uwanja wa taifa, halikadhalika mchezo wa Mbeya City dhidi ya Azam FC katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mbeya City Fc hawana rekodi nzuri kwa Azam FC hususani katika dimba la Sokoine kwa kuwa wamekuwa wakifungwa na Azam mara kwa mara
nyumbani kwao. Kwa maana hiyo tunaamini mchezo huo utakuwa na upinzani wa hali ya juu kwa sababu Azam naye atataka kuendeleza historia yake ya kumuonea Mbeya City katika dimba lao la nyumbani.
0 comments:
Post a Comment