MSHAMBULIAJI wa Uganda, Geoffrey Massa bado ana matumaini kuwa The Cranes inaweza kufanya vizuri katika mchezo wake wa marudiano kuwania kufuzu AFCON 2015 utakaopigwa leo dhidi ya wenyeji Togo.
Uganda wanakabiliana na Togo katika uwanja wa Stade de Kégué na wana matumaini ya kuwafunga wenyeji kwa mara ya kwanza katika mechi sita walizokutana ili kuongeza matumaini ya kufuzu Afcon mwakani nchini Morocco.
Massa ambaye anabeba matumaini ya Waganda wengi anatarajia kufunga goli akati huu muhimu ambao nahodha wao Andy Mwesigwa anatumikia adhabu.
"Kama ulivyosema, mimi na Tonny (Mawejje) na Dennis (Onyango), tumekuwa tukicheza katika timu hii kwa miaka mingi," Alisema Massa ambaye atakuwa nahodha katika mechi ya leo mjini Lome, Togo.
"Tunahitaji kuwaongoza wenzetu, tulipoteza mechi jumamosi, hatujapata nafasi nzuri ya kujirekebisha na tunacheza kesho (leo), hivyo ni kupambana tu".
Uganda walipoteza mechi ya kwanza mjini Kampala kwa bao 1-0 na wanahitaji matokeo mazuri ugenini ili kuendeleza matumaini yao ya kufuzu fainali za mataifa ya Africa.
0 comments:
Post a Comment