Maneno yanayo onekana katika picha ya basi la simba "KILIMO KWANZA" na "BUNJU" ni maneo ambayo hayapo katika mabasi halisi ya Simba Sc. |
Amini usiamini mechi ya Simba na Yanga (Dar Derby), ni mchezo wenye hisia kali sana kwa mashabiki wa timu hizi mbili, tofauti na timu hizi zinapocheza na timu zingine.
Nimekuwa nikiwafuatilia mashabiki wa timu hizi mbili kwa ukaribu katika mitandao ya kijamii hususani Face book, ndipo nikagundua hali imefikia patamu sasa kwani licha ya mashabiki hawa "Simba vs Yanga" kutumia misemo mbalimbali ya kukejeliani, wameona hiyo haitoshi na sasa wameanza kwenda mbali zaidi kwa kutumia ubunifu wa kuhariri picha (picture editing) ambazo hurushwa katika mitandao ya kijamii kila mmoja akijitamba na timu yake.
Kwa sasa Simba Sc klabu bado ipo Afrika ya kusini ikijiwinda na mchezo huo wa watani wa jadi ambao utafanyika siku ya Juma mosi Oct 18, 2014 katika uwanja wa taifa Dar es salaam, wakati huo huo Yanga Sc klabu nao wapo hahapa mjini maeneo ya Boko ambapo hufanya mazoezi yao kila siku katika uwanja wa Boko Veterans.
0 comments:
Post a Comment