Huenda adhabu kali kutoka UEFA ikawapata mashabiki wa klabu ya Galatasaray kwa kutupa
mafataki (flares) uwanjani wakati wa mechi yao dhidi ya Arsenal, mchezo ambayo ulipigwa katika dimbani la Emarates na Arsenal kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya klabu hiyo ya Galatasaray yenye makazi yake jijini Instanbul nchini Uturuki.
|
Usiombe kukutana na mashabiki wa Galatasaray, mwangali huyo shabiki mmoja Galatasaray akiporomosha litusi la kidole kwa wachezaji wa Arsenal huku wenzake wakimshangilia |
|
Pichani ni mlinda lango wa Galatasaray, Fernando Muslera akijaribu kuondoa moja ya fataki iliyorushwa uwanjani na mashabiki wa timu yake. |
Mashabiki wa Galatasaray ambao wanasifika kwa uzalendo mkubwa walionao na timu yao hiyo, walianza kurusha mafataki ndani ya uwanja dakika ya 36 ya mchezo, mara baada ya kuona timu yao imezidiwa na Arsenala baada ya timu hiyo kuwa mbele kipindi cha kwanza kwa magoli 2-0, magoli ambayo yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck.
|
Ilikuwa ni shughuli pevu kwa upande wa maafisa wa usalama kuwatuliza mashabiki hao dimbani Emarates. Mpaka hivi sasa watu sita wanashikiliwa rumande kwa tuhuma za kuhusika na usumbufu huo. |
Hata hivyo hamsha hamsha hiyo ya mashabiki ambao ulifanya mchezo usimame kwa dakika kadhaa, iliweza kuthibitiwa mara moja na ma-afisa usalama waliokuwepo uwanjani hapo ingawaje mashabiki wa Galatasaray baadaye waliendelea kupiga
mafataki hayo nje ya uwanja wa Emarates baada ya mtanange huo.
Kwa upande wa idara ya nidhamu ya UEFA, imesema itachukua hatua stahiki kwa mashabiki hao kwani ni kosa kisheria kutupa vitu ndani ya unja wakati wa mchezo.
Mbali na kuwa na heshima kubwa, mashindano ya Mabingwa barani Ulaya (CL) huwa na faida kubwa sana kwa klbu kwani ni moja ya ligi inayotoa pesa nyingi kwa timu shiriki halikadhalika kwa timu itakayo nyakuwa ubingwa.
0 comments:
Post a Comment