Kutoka kushoto Saimon Msuva Geilson Santos Santana 'Jaja' na Mrisho Ngassa
KOCHA mkuu wa Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo
amekazania kuwafundisha wachezaji wake namna ya kumiliki mpira, kupiga pasi za
uhakika, kushambulia kwa kasi na kujilinda vizuri kuelekea katika mechi ya
watani wa jadi ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Simba sc itakayopigwa
Oktoba 18 mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Maximo ambaye anakinoa kikosi chake katika uwanja
wa Boko Veterani uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam amejikita zaidi kuwaandaa mawinga wake
hatari, Mrisho Khalfan Ngassa ‘Anko’ na Saimon Happygod Msuva ili kuwaua
mahasimu wao wanaonolewa na kocha Mzambia, Patrick Phiri.
Mbrazil huyu mwenye heshima kubwa hapa nchini
imeonekana kuwaandaa Ngassa na Msuva kwa muda mrefu, na hii inamaanisha
atashambulia zaidi akitumia mawinga wa pembeni wenye kasi kubwa.
Ngassa na Msuva kwa muda mrefu wamekuwa
wakifundishwa kupiga krosi kali zenye madhara langoni, huku nao Nizar Khalfan,
Hussein Javu na Andrey Coutinho wakifundishwa zoezi hilo kwa muda mrefu.
Wakati Yanga wakiwa Dar, Simba wao wapo bondeni‘Sauzi
Afrika’ wakinoa makali yao.
0 comments:
Post a Comment