Klabu kongwe na pendwa zaidi duniani, Manchester United imekamilisha makubaliano yao binafsi na mshambuliaji wake mpya Mkolombia, Radamel Falcaohave ikiwa ni mazingira ya kuhakikisha hakutatokea mgogoro wowote baadaye endapo wataamua kumpa Falcao mkataba wa kudumu Old Trafford.
Falcao ni mmoja wa wanandinga wenye rekodi ya majeraha ya mara kwa mara |
Falcao 28, ametua kunako Manchester United kwa ada ya mkopo ya pauni milioni 6 kutoka FC Monaco ya Ufaransa saa chache kabla ya dirisha kubwa la usajili kufungwa July Mosi, 2014.
Kwa mujibu wa katibu mkuu mtendaji wa Manchester United , Ed Woodward alisema, mpaka sasa wameshakubaliana na FC Monaco kulipa kiasi cha Pauni milioni 43.5 endapo watakubali kumpa Falcao mkataba wa kudumu klabuni hapo baada ya msimu huu wa ligi kuu Uingereza kumalizika na hakutatokea madiliko yoyote ya kiwango hicho cha pesa.
Manchester United, wameamua kuweka sawa mambo hayo haraka ili kuzuia purukushani iliyowakuta 2009 baada ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji CarlosTevez kutoka West Ham United na baadaye kukubali kubaki naye kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 25, lakini dili hilo likabuma kwa kuwa Tevez hawakuridhiani maridhiano binafsi na Man U (personal terms) ambapo aliamua kutimukia kwa mahisumu wao wa jadi Manchester City.
Kwa sasa Falcao anatumikia Mashetani Wekundu kwa makubaliano ya kutafuna kitita cha pauni milioni 250,000 kwa wiki mbali na marupurupu yanayotokana na haki za matangazo.
0 comments:
Post a Comment