Mpambano mkali wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika
October 25 katika ukumbi wa
friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa
habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi
nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
amesema kuwa siku hiyo kutakuwa
na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi
Mbelwa 'Moto wa Gesi' na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha
Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa
hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea
umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano jingine ni kati ya Juma
Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana
kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola
anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu
Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver
na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi
atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed
Mbishi
Katika mpambano huo siku hiyo
kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika
swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu
utapambwa na burudani mbalimbali
siku
hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha
mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka
kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya
mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny
Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
0 comments:
Post a Comment