Saturday, October 11, 2014

Luis Suarez alikuwa muhimili mkubwa sana kwa upande wa timu ya taifa ya Uruguay, wakati timu hiyo ikitoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Saudi Arabia  katika mechi ya kirafiki ya kimataifa uliopigwa jana katika dimba la Prince Abdullah al-Faisal nchini Saud Arabia.
Uwezo aliokuwa anaonyesha jana Suarez uwanjani, ni faraja kubwa sana kwa kocha wa Barcelona FC, Luis Enrique ambaye anategemea kumtumia nyota huyo katika mechi ya El clasico ( Barcelona vs RealMadrid) Octoba 25, 2014
Suarez Alipiga shuti kali lilogonga mwamba na  kumbabatiza beki wa Saudi Arabia kisha baadaye kuzama nyavuni na kufanya Uruguaya kuongoza katika mchezo huo mpaka pale goli hilo lilopo sawazishwa dakika za majeruhi na mshambuliaji Saud Arabia, Naifu Hazazi.
Luis Suarez alipigwa marufuku kushiriki mashindano yoyote kwa muda wa miezi minne pamoja na adhabu ya kutoshiriki mechi 9 za kimataifa baada ya kumg'ata beki wa timu ya taifa ya Italy, Giorgio Chiellini wakati wa michuano ya komba la dunia 2014. Adhabu zake zote zinatarajiwa kumalizika Octoba 25, 2014

Kwa upande mwingine, Giorgio Chiellini "kitoweo cha Suarez" jana alifungia timu yake ya taifa magoli 2-1 wakati ilipokuwa ikipepetana dhidi Azerbaijan. Chiellini ndiye amewasaidia Azerbaijan kupata goli baada ya kujifunga.
 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video