Kulia ni kocha mkuu wa West Ham akipongezana na kocha wa Man U Van Gaaal baada ya mechi yao ya Jumamosi iliyopita, Sep 28, 2014 |
Allardyce alisema enzi za kibabu Fergie mambo yalikuwa burudani Old Trafford kwani kibabu alikuwa akitenga muda mfupi wa kuteta na kocha wa timu pinzani baada ya mechi huku wa wakipata kinywaji.
"Baada ya mechi kama nilivyozoea nilielekea katika chumba ambacho Ferguson zamani alikuwa akipenda kukutana na makocha wa timu pinzani kupata kinywaji baada ya mechi kwa siku husika huku wakibadilishana mawazo, lakini nilishangaa sana kuambiwa ule utaratibu haupo tena, kiukweli nilitoka na aibu kubwa ukizingatia nimefungwa magoli 2-1 siku hiyo!" Allardyce alisema.
Baada ya kupoteza mchezo huo dhidi ya Man U wikiendi iliyopita, West Ham sasa wako katika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza huku Mashetani Wekundu wakiendelea kuienzi mtaa wa saba (nafasai ya saba) ambayo ndiyo ilikuwa nafasi yao mpaka ligi ya msimu wa 2013/2014 inamalizika
0 comments:
Post a Comment