Kutoka kulia ni mwenyekiti wa Yanga Sc Wilaya ya Kahama Bw. Museveni na mwingine ni Maximo katika harakati za kufungua tawi hilo. |
Baada ya mazoezi ya leo asubuhi, Octoba 29,2014, kocha mkuu wa yanga, Marcio Maximo akiwa na baadhi ya voiongozi wa klabu hiyo alipata fursa ya kuzindua tawi jipya la Yanga Sc mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Yanga ilimaliza mechi yake ya tano ya duru ya kwanza ya ligi kuu Tanzania Bara msimu huu kwa kuichapa Stand United magoli 3-0 wikiendi iliyopita mkoani Shinyanga, lakini wakaamua kuendelea kuweka kambi mkoani humo kujiweka sawa kabla ya kuelekea katika kipute kingine Jumamosi ijayo dhidi ya Mtibwa sugar ya Morogoro ambayo ndiyo kinara wa ligi hiyo kwa sasa.
Wakiwa mkoani humo timu ya Yanga imepta nafasi ya kucheza mechi za kirafiki na timu za daraja mbalimbali ikiwemo timu ya Ambassador Fc ya mjini kahama
Kwa sasa Yanga ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bar 2014/15 wakiwa wamejikusanyia alama 10 kibindoni sawa na wapinzani wao Azam Fc, utofauti wao ukiwa ni idadi ya magoli ya kufunga na ya kufungwa.
0 comments:
Post a Comment