Baada ya jana Barcelona FC kumtandika Eibar magoli 3-0 , kocha wa Barcelona, Luis Enrique amesema kwamba bado haamini kama matokeo hayo ni tafsiri sahihi ya kitakachotokea Jumamosi Oct 25, 2014 watakapo kutana na Real Madrid dimbani Estadio Santiago Bernabeu.
"Malengo yetu ni kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu Jumamosi dhidi ya Real Madrid kwenye mchezo mzuri "El Clasico" utakao wakutanisha mahasimu wakubwa wa kandanda nchini Hispania, kumbuka endapo tukishinda maana yake ni kwamba tutazidi kujikita kileleni mwa ligi huku tukiwa tumemuacha mpinzani wetu mkubwa Real Madrid kwa jumla ya point saba.
"Lakini, kwa upande wangu bado naona matokeo ya aina yeyote katika mechi ya Jumamosi bado haitoa tafsiri halisi ya nani atakuwa bingwa wa Laliga kwa kuwa bado ligi ni mbichi kabisa, ila pamoja na hayo yote Wakatalunya sisi tunahitaji alama tatu muhimu Jumosi". Hiyo ndiyo kauli ya Luis Enrique jana baada ya mechidi ya Eibar.
Kumbuka katika hiyo mechi ya Jumaosi "El Clasico", ndiyo Barcelona wanatarajia kumtumia kwa mara ya kwanza mshambuaji wao Luis
Suarez ambaye amekuwa nje ya dimba kwa muda wa miezi minne akitumia adhabu ya utovu wa nidhamu. FIFA ilimfungia Suarez kucheza mpira kwa miezi minne baada ya kumg'ata beki ya Italy Giorgio Chiellini wakati wa michuano ya kombe la mwaka huu nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment