Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015 inaanza kutimua vumbi kesho (Oktoba 11 mwaka huu) katika viwanja tisa tofauti kwenye miji ya Moshi, Arusha, Musoma, Mwanza, Geita, Mbozi, Songea, Mufindi na Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kamati ya mashindano ya TFF, Boniface Wambura akitoa taarifa kuhusu kuanza kwa ligi daraja la kwanza Tanzania bara msimu wa 2014/2015 katika ofisi za TFF leo. |
Kundi A litakuwa na mechi kati ya Kimondo FC na Villa Squad itachezwa Uwanja wa Vwawa mjini Mbozi wakati Majimaji itaumana na Ashanti United (Uwanja wa Majimaji, Songea).
Nyingine ni Kurugenzi Mafinga na Tessema FC kwenye Uwanja wa Mufindi huku Friends Rangers ikioneshana kazi na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Kundi B ni Panone itaikabili Kanembwa JKT (Uwanja wa Ushirika, Moshi), Oljoro JKT itapambana na Polisi Dodoma (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abedi, Arusha), Polisi Mara na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Musoma).
Mechi nyingine ni kati ya Toto Africans na Mwadui itakayofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na Geita Gold na Burkina Faso (Uwanja wa Waja, Geita).
0 comments:
Post a Comment