Kibadeni enzi hizo akiifundisha Simba sc
WINGA machachari na kocha wa zamani wa Simba sc,
Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Abdallah Kibadeni Mputa’ amesema hataki tena
presha ya kufundisha klabu za ligi kuu soka Tanzania bara.
Akizungumza katika mahojiano maalum na mtandao
huu, Kibadeni aliyeiongoza Simba mzunguko wa kwanza msimu uliopita kabla ya
kurithiwa na Zdravko Logarusic alisema anajenga akademi yake maeneo ya Chanika
jijini Dar es salaam ambapo atakuwa anafundisha soka vijana wadogo.
Akademi hiyo itakayojulikana kwa jina la ‘Kibadeni
Soccer Academy’, KISA itakuwa inachukua vijana kutoka maeneo mbalimbali.
Kibadeni mwenye rekodi ya pekee ya kufunga mabao
matatu ‘Hat-trick’ katika mechi ya watani wa jadi mwaka 1977 ambayo haijavunjwa
mpaka leo alisema amechoshwa na dharau za baadhi ya wadau wa michezo hasa
wanaposema hajasomea mpira wakati alikwenda Ujerumani na Brazil kupiga shule.
Akizungumzia mechi ya watani wa jadi Oktoba 18
mwaka huu, Kibadeni mwenye rekodi ya pekee Afrika mashariki na kati kwa kuifikisha
Simba fainali ya kombe la CAF mwaka 1993 alisema ni mechi ngumu, timu
itakayocheza kwa umakini itaweza kushinda, lakini hawezi kutabiri matokeo.
Hata hivyo alishangazwa na sare tatu walizopata
Simba katika mechi tatu za kwanza akisema haoni sababu ya matokeo hayo
kwasababu wamesajili wachezaji wakali.
“Sielewi kinachowakumba, kwa uongozi thabiti walionao,
usajili waliofanya, nashangaa kuona wanapata matokeo kama haya. Nadhani kuna
sehemu wamekosea, labda kuna watu wanawaombea dua mbaya kwasasa waliwafanyia
vitu vibaya”. Alisema Kibadeni.
0 comments:
Post a Comment