Mlinda lango wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Iker Casillas ndiye bado anashikilia rekodi ya kuwa mlinda lango anayelipwa pesa nyingi duniani kwa kazi hiyo. Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na jarida la The Richest la mwaka 2014.
Casillas anakula kitita cha pauni milioni 6.30 kwa mwaka sawa na bilioni 1.26 pesa za kitanzania kwa mwaka. Casillas ni mmoja wa walinda lango wanoheshimiwa sana nchini Hispania na ndiyo maana ni nahodha wa klabu yake ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, pengine ni kwa sababu ni zao la football academy za nchini humo.
Iker Casillas alikuwa mlinda lango wa timu ya taifa ya Hispania wakati timu hiyo inachukuwa ubingwa wa mataifa ya Ulaya mwaka 20008 baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa takriban miaka 44 iliyopita. Mbali na mafanikio hayo, goli kipa huyo pia alisaidia Hispania kuchukuwa kombe la dunia mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment