Ama kweli "Mechi ya Watani wa jadi" siyo mchezo hata kidogo. Baada ya kuona maandalizi makubwa yanayofanywa na mahasimu wao Simba Sc kuelekea katika mchezo wa watani wa jadi (nani mtani jembe ) Oct 18, 2014, Dar es Salaam Young Africans nao wamecharuka leo hii na kuammua kuanza kambi yao katika hoteli ya kifahari ya LandMark iliyopo mitaa ya Kunduchi jijini Dar es salaaam kuhakikisha wanajiweka sawa kwa kipute hicho.
Kikosi cha wachezaji 28 chini ya kocha mkuu wa klabu hiyo, Marcio Maximo ndicho kilicho ingia kambini ambapo kitakuwa kikifanya mazoezi katika uwanja wa Boko- Boko Veterans asubuhi na jioni.
"Namshukuru Mungu vijana wangu wote wapo fiti kiafya, kifikra na pia wanaonekana kuwa na morali ya hali juu sana kuelekea katika hiyo 'Dar es salaam derby' Oct 18, 2014
"Tunafahamu kwamba mchezo wa watani wa jadi siku zote huwa mgumu sana, lakini sisi kama Yanga tumelitambua hilo na ndiyo maana tunajipanga vyema kuhakikisha siku hiyo tunachukua ubingwa tena kwa kishindo dhidi ya Simba Sc" Alisema Maximo.
Kuhusu wale wachezaji saba waliokuwa katika kambi ya Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Benin, tayari wamesha ungana na wachezaji wengine kambini leo, na cha kushukuru zaidi hakuna majeruhi wa aina yeyote.
Hwa ndiyo wachezaji walio ingia kambini:
Walinda lango: Juma Kaseja, Ally Mustapha 'Bartez' na Deo Munishi 'Dida'
Walinzi: Juma Abdul, Salim Telela, Oscar Joshwa,Amos Abel, Edward Charles, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Kelvin Yongani na Nadir Haroub 'Canavaro'
Viungo: Mbuyu Twite, Said Juma 'Makapu', Omega Seme, Hamis Thabit, Nizar Khalfani, Issa Ngawo na Haruna Nionzima.
Washambuliaji: Geilson Santos 'Jaja', Andrey Coutinho, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza, Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Husein Javu na Jerson Tegete.
0 comments:
Post a Comment