Kwa sasa Ruvu Shooting wanaburuza mkia katika msimamo wa ligi ya VPL 2014/2015 wakiwa wamepoteza michezo yote miwili ya awali na hawana pointi yoyote. |
Kwa matokeo hayo ya awali, hakuna ubishi kwamba, Ruvu shooting msimu huu hawana wachezaji wazuri, na kama wana wachezaji wazuri basi, benji la ufundi halijafanikiwa kuteua wachezaji wenye uwezo kwa ajili kushindana kupata ushindi. Mpaka sasa ni vigumu kusema Ruvu shooting wana nafuu katika idara gani kwani hawaezi kufunga magoli, lakini pia wanaruhusu magoli mengi.
Akilonga na mtandao huu, msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ( Bwana Mipasho) alisema wamechoshwa na matokeo duni ya mechi za awali za ufungizi wa ligi tena katika uwanja wa nyumbani.
"Ndugu yangu, nachoweza kusema ni kwamba sisi Ruvu Shooting hatuja pendezwa na matokeo ya mechi mbili zilizopita ambazo tulipoteza. Lakini, tumetambua matatizo yetu na kikosi chetu chini ya kocha bora, Tom Olaba kimeanza kufanya marekebisho muhimu ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mechi yetu dhidi ya Mbeya City siku ya Jumamosi". Masau alisema.
Lakini kwa upande wake kocha mkuu wa Mbeya City FC, Juma Mwambusi, amesema mechi ya leo dhidi ya Ruvu Shooting ni mchezo muhimu sana kwao kwa kuwa ni mchezo wa kwanza wakiwa ugenini msimu huu na wangependa kupata ushindi ili kuendelea kujiweka vizuri katika msimu wa ligi.
Hata hivyo nao, Mbeya City Fc hawako katika kiwango cha kusisimua kama ilivyokuwa msimu wa jana, kwani kati ya michezo miwili ambayo wamekwisha cheza, wametoka suluhu na Ruvu Stars na kushinda goli 1-0 dhidi ya Costal Union tena kwa mbinde.
Huu utakuwa ni mchezo wa kukamia zaidi leo katika dimba la Mabatini, kwani Ruvu Shooting watataka kurudisha imani kwa mashibiki wake, lakini nao Mbeya City watataka kulinda sifa yao nzuri ya kuwa timu chipukizi bora ya msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment