Sunday, October 5, 2014

Hii ni historia nyingine kwa klabu ya Simba katika ligi kuu Tanzania Bara kutoa sare michezo mitatu mfululizo uwanja wa nyumbani. Ni hisotoria ambayo pengine haikuwahi kutokea na kama imewahi basi ni kitambo sana kiasi ya wengi wetu kutoweza kukumbuka.

Mara nyingi timu inapofanya vibaya, watu hususana wapenzi na mashabiki  huanza kumsaka mchawi wao ni nani, awe ndani ya uwanja au nje ya uwanja na ndicho kinachotoke sasa katika klabu ya Simba, moja ya klabu pendwa zaidi nchini.

Kulia ni kiungo wa mshambuliaji wa Simba, Kisiga akijaribu kumtoka beki wa Stand United, Reyna Mgungira katika mpepetano wa jana  uwanja wa taifa Dar es salaam
Baada ya ligi kuanza Sep 20,2014, Simba SC ilianza ligi  kwa kutoa sare ya magoli 2-2 dhi ya Wagosi wa Ndima, Costal Union ya jijini Tanga. Hilo halikuwasumbua sana wanasimba kwa kuwa waliamini ni mambo ya kawaida katika mpira wa miguu ingawaje hawakuridhishwa na jinsi magoli yale yalivyo sawazishwa na Costal Union kwani magoli yote yalirudi kipindi cha pili na waliponea chupuchupu kupigwa goli la tatu dakika za majeruhi.

Pia, katika mchezo wao wa pili dhidi ya Polisi Morogoro, Simba walijikuta wakilazimishwa tena sare nyingine ya goli 1-1.Kitendo hiki kiliwachanganya zaidi wapenzi wa klabu ya Simba ambapo maneno kama "Simba Ukawa" yalianza kusikika mitaani. Je Simba Ukawa ni akina nani?

Jibu ni rahisi "Simba ukawa" ni wale wanachama 71 wa Simba  akiwemo Michael Richard Wambura waliofutiwa uwanachama kwa sababu mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuipeleka Simba Sc mahakama za kawaida kinyume cha sheiria. Je, "Simba Ukawa" ndiyo kweli wanasababisha Simba kupata matokeo yasiyo ridhisha?

Jibu lipo wazi, kwa jicho la kitaalamu "Simba Ukawa" hawa husiki hata kidogo na kiwango duni kinacho onyeshwa na Simba. Kama jana ulifutalia vizuri mchezo wa tatu wa Simba SC dhidi ya Stand United ya Shinyanga ambayo pia walitoka sare ya goli 1-1 katika dimba la taifa, utagundua kabisa kwamba tatizo la Simba lipo katika benji la ufundi na wachezaji. Ki vipi?

Kuna msemo usemao ndege wanofanana huruka pamoja, kiufundi hii ina maana kwamba katika timu ya Simba  kuna utofauti mkubwa kutoka mchezaji mmoja kwenda kwa mchezaji mwingi kiuezo wa kusakata kabumbu. Wachezaji wenye uwezo ni wachache mno.

Wachezaji wenye uwezo wa kufunga magoli Simba ni mshambuliaji Hamisi Tambwe pamoja na kiungo mshambuliaji Shaaban Kisiga, mbali na hao wengine siyo wakutegemewa kabisa. Lakini mara nyingi tunamuona kocha Patrick Phiri akifanya mabadiliko ya kumtoa Tambwe au Kisiga na mmoja kati ya hawa akitoka inakuwa ni ngumu kwa Simba kupata goli, fuatilia michezo yote mitatu aliyo cheza Simba utagundua hilo.Maana yake kuna maelewano mazuri kati ya Tambwe na Kisiga

Mbali na hilo pia, mabeki wa Simba ni wazuri lakini hawana masiliano (communication) magoli wanayofungwa, mengi ni yale ya kukosa mawasiliano. Hakuna kioungozi katika hiyo idara anaye wahamasisha wenzake kuwa makini muda wote wa mchezo.

Suala lingini linaloisumbua Simba ni Ugeni wa wachezaji wengi tegemeo klabuni hapo hususani katika safu ya ushambuliaji na falsafa mpya kutoka kwa kocha mpya Patrick Phiri ambaye amekabidhiwa timu takriban  mwezi mmoja kabla ya  ligi kuanza.

Kwa kuwa Phiri ni mgeni (mpya) klabu hapo ni wazi kwamba wachezaji aliowakuta siyo wachezaji aliyo wapendekeza yeye, kwa hiyo inakuwa ni vigumu kuanza kuwatumia wachezaji ambao hawakusajiliwa kulingana na falasafa au mbinu zako. Hii pia inakuwa ni ngumu kwa mwalimu kuwabadilisha wachezaji wa aina hiyo waendane na mfumo wake na kupata matokeo mazuri kwa haraka. Inahitajika wanasimba kuwa watulivu na kuweka mikakati dhabiti kwa mustakabli wa klabu yao na kuwachana kabisa na maamuzi ya kukurupuka.

Lakinini tukiachana na Simba, ni wazi kwamba timu nyingi za msimu huu zimejiandaa vizuri na zimekuja kiushindani kabisa tofauti ni mategemeo ya wengi.








0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video