Klabu ya Arsenal ndiyo inashikilia rekodi kwa tiketi zake za msimu kuwa juu, inakadiriwa kuwa ni kati ya pauni 1,014 hadi pauni 2,013 kwa msimu |
Kwa mujibu wa ripoti liliyotelewa hivi karibuni na shirika la habari la kimataifa BBC kupitia kitengo chake maalumu cha "BBC Sport Price of Football", zinaonyesha kwamba, gharama za kutazama mechi za ligi kuu nchini Uingereza kwa msimu zimepanda kwa takribani mara nne tangu mwaka 2011-2014, huku tiketi za klabu ya Arsenal za msimu zikiongoza kuwa ya bei ya juu mno ukilinganisha na klabu zingine za nchini humo.
Inadaiwa kwamba bei ya chini kabisa kwa sasa ya kushuhudia mechi yeyote ya siku katika ligi zote nne za nchini Uingereza ambazo ni rasmi, ikiwemo ligi kuu ni pauni 29 sawa na shilingi za kitanzania 58,000/= kwa kichwa. Maana yake ni kwamba gharama hizo zimepanda kwa asilimia 13 zaidi ukilinganisha na gharama za maisha ya kawaida nchini Uingereza ambayo yenyewe yamepanda kwa asilimia 6.8.
Ripoti inaonyesha kwamba tiketi za ligi kuu chini Uingereza zimepanda kwa wastani wa pauni 508 kwa msimu zaidi ukilinganisha na za Bundesliga (Ujerumani) ambayo wastani wake ni pauni 138 kwa mwaka. Kiwango cha chini anacholipa shabiki wa Ujerumani kutazama mechi kwa siku husika ni pauni 109, wakati huko Hispania ( Laliga) shabiki anaweza kupata tiketi ya msimu kwa pauni 103 tu.
Lakini kwa upande mwinge, ripoti hiyo pia imeonyesha kwamba, tiketi za bei ya chini za mechi kwa siku husika (Match-day price) za klabu ya Chelsea dimbani Stanford Bridge ni pauni 50, hali inayofanya tiketi za mechi ya siku husika ya Chelsea kuwa ghali zaidi nchini Uingereza.
0 comments:
Post a Comment