Na Mwandishi Wetu, Tanga
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema utakwenda
mahakamani kuishtaki Kampuni ya Binslum Tyre kutokana na kitendo cha
kutengeneza tisheti za Coastal Union zenye nembo ya kampuni Sound na kuwapa
bure mashabiki kuingiza nazo kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara
wakiwa wamelipiwa na viingilo vya mchezo husika.
Hali
hiyo ni kinyume na utaratibu kutokana na kuwa tayari kampuni hiyo ilishajitoka
kufadhili timu hiyo na tayari klabu ya Coastal Union ilikwishapata mfadhili
mwengine ambayo ni kiwanda cha Kutengeneza Unga Ngano mkoani Tanga cha Pembe
Flours Mills.
Kauli
hiyo imetolewa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji Kilichoketi mwishoni mwa
wiki ambapo kilikuwa na agenda nne za msingi ambazo ni Suala la mshambuliaji wa
Coastal Union Danny Lyanga,Utoaji slipi benki,Jezi za Sound,Tarehe ya Uchaguzi.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na viongozi wa mbalimbali akiwemo makamu Mwenyekiti wa Klabu ya
Coastal
Union,Steven
Mguto,Katibu Mkuu Kassim El Siagi,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji,Albert Peter
Saimu Amiri na Meneja wa Coastal Union Akida Machai.
Kimsingi
suala ambalo lilikuwa gumzo ni suala la kampuni hiyo kuchukua hatua ya
kuwavalisha mahsbiki wa Coastal Union jezi pamoja na kuwalipia viingilio vya
mechi kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu.
Kama
unavyojua kuwa Kampuni ya Binslum Tyres ilikuwa mhisani wetu na sasa hatuko
naye na tayari alishapeleka fedha zake kwenye vilabu vingine ikiwemo Mbeya City
sasa tunamshangaa kuendelea kufanya biashara ya matangazo kupitia mashabiki
wetu kwa kuwapa tisheti za kuvaa bure ikiwemo kuwalipia viingilio kwenye mechi
za ligi kuu zinazochezwa Mkwakwani.
Hivyo
kutokana na suala hilo tayari uongozi wa Coastal Union umeshamkamata mshabiki
mmoja ambaye ni wakala wa kusambaza tisheti hizo kwa mashabiki na kumpeleka
polisi na taratibu za kisheria zinaendelea ili kuweza kukomesha vitendo hivyo
ambavyo sio vya kiungwana.
Tayari
Kampuni ya Pembe Flours Mills ilishasaini mkataba na Klabu ya Coastal Union wa
kufadhili kwa kipindi cha mwaka mmoja hivyo Kampuni hiyo kuendelea kufanya matangazo
yake kupitia mashabiki hao ni kuvunja utaratibu uliokuwepo.
Hata
hivyo tayari Pembe walishatoa jezi 2000 kwa ajili ya kuziuza kwa masabiki
mbalimbali wa soka jijini Tanga zilizokuwa na nembo ya pembe na TSN.
Kuhusu
suala la Uchaguzi wajumbe wa Kamati hiyo walikubaliana uchaguzi huo ufanyika
Novemba 23 mwaka huu ambapo nafasi zitakazojazwa ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo na
wajumbe wawili wa kamati ya utendaji
Suala
la Utiliaji Sahihi wajumbe walilipendekeza fedha zitumike kwenye matumizi
yanayofahamika ikiwemo kuwekwa utaratibu wa wazi kwenye matumizi husika.
0 comments:
Post a Comment