Kikosi cha leo cha Nigeria; walihitaji ushindi wa aina yoyote ili kujiweka katika hali nzuri lakini ilishindikana kabisa. |
Bingwa mtetezi wa kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), Nigeria, leo ameonja joto la jiwe baada ya kujikuta wakibanwa mbavu na Sudan kwa kuchapwa goli 1-0. Goli hili linaifanya timu ya taifa ya Nigeria chini kocha wa Stephene Keshi kuburuza mkia katika kundi lao lenye timu za Congo Brazaville na Afrika Kusini.
Sudan walipata goli la kwanza na la ushindi mnamo dakika za mwisha wa kipindi cha kwanza ya mpepetano huo kupitia mshambuliaji wao, Bakri Almadina
0 comments:
Post a Comment