Friday, October 24, 2014

Baada ya Baloteli kujiunga na klabu ya Liverpool akitokea AC Millan ya nchini Italy mwishoni mwa dirisha kubwa la usajili 2014/2015, aliagiza aletewe gari lake hilo kwa njia ya meli kutoka Italy kwenda Uingereza.
Wakati mtukutu Super Mrio Baloteli akisubiri adhabu kutoka kwa kocha wake, Brendan Rodgers kwa kosa la kubadilishana jezi na Beki wa Real Madrid 'Pepe" Juma tano

iliyopita kabla mechi haijaisha, Baloteli amekutana na kisanga kingine dhidi ya maafisa wa polisi jijini Manchester baada ya kumtishia mwanamke mmoja aliyekuwa akijaribu kupiga picha gari lake la kifahari akiwa njiani kuelekea kwa mama yake jijini humo.

Baloteli alikuwa jijini Manchester ambako alikwenda kumsalimia mama yake anayefahamika kwa jina la Rose Barwuah ambaye anaishi mitaa ya Wythenshawe jijini humo, lakini ghafla akiwa njiani kuelekea kwa mama yake, alimuona mwana dada mmoja akiwa bize kupiga picha gari lake aina ya Ferrari 12 Berlinetta ambalo gharama yake inakdariwa kuwa ni paundi 240,000 sawa na milioni za kitanzania  mia nne themanini (480,000,000).

Katika hali isiyotarajiwa, Baloteli alianza kumkemea dada yule huku akimtishia kumpiga makofi endapo angeendelea kufanya hivyo, kitendo kilichomfanya dada huyo kwenda polisi kushitakiki kwa kutishiwa maisha na Baloteli.

Great Manchester Police (GMP), wamesema wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu suala hilo kisha watamchukulia Baloteli hatua endapo atakuwa na hatia ya kutishia maisha ya watu. 

Hilo linakuwa ni janga la pili kumpata Baloteli wiki hii ambaye anasubiri adhabu kutoka kwa kocha wake Brenda Rodgers kwa kosa la kubadilisha jezi kabla ya mechi kumalizi katika mechi ya Jumatano iliyopita ambayo Liverpool ilipigwa magoli 3-0 dhidi ya miamba ya soka wa Hispania, Real Madrid.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video