Hivi ndivyo mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam FC "Matajiri wa Dar" wanavyojifua katika moja ya fukwe maarufu hapa jijini Dar es salaam "Coco Beach" kuhakikisha wanaendelea kuwa moto wa kuotea mbali katika ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mtandao wa klabu ya Azam; zimedhibitisha kuwa wachezaji wote wako salama na wala hakuna majeruhi wapya. Wamedhibitisha kwamba Kelvin Friday ambaye alikuwa majeruhi yuko fiti kwa mchezo ujao dhidi ya Mbeya City [Picha: Azama fc] |
Azam FC ni moja kati ya timu za ligi kuu Tanzania Bara ziliyofanikiwa kuanza ligi kuu vizuri, wamesha cheza michezo mitatu ambao wameafanikiwa kushinda michezo miwili; mchezo wa kwanza wa ufunguzi walimpiga Polisi Morogoro maogli 3-1, mchezo wa pili dhidi ya Ruvu shooting, walishinda kwa mgoli 2-0 na mchezo wa hivi karibuni walitoka suluhu dhidi Tanzania Prisons ya huko Mbeya. Kwa sasa "Walamba koni" wapo katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa na alama saba, alama mbili nyuma ya vinara wa ligi hiyo kwa sasa Mtibwa Sugar ambao wana alama tisa mkono.
Ligi kuu itaendelea tena hapo Octoba 18, 2014 kwa mechi sita kupigwa, ambapo Azam Fc watasafiri kuelekea Mbeya kupepetana na wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, Mbeya City FC katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine.
0 comments:
Post a Comment