MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Togo,
Emmanuel Adebayor yuko safarini kwenda Kampala tayari kwa mechi ya wiki hii ya
kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika, Afcon 2015 dhidi ya Uganda The
Cranes.
Siku chache zilizopita Adebayor
hukuwepo kwenye kikosi cha Togo wakati wa mazoezi mjini Lome na hali hii ilizua
wasiwasi kwamba angekosa mechi hiyo muhimu.
Hata hivyo, Supersport.com
imethibitisha kuwa nyota huyo anayekipiga klabu ya Tottenham inayoshiriki ligi
kuu soka nchini England amekuwepo Uganda asubuhi ya leo akitokea Nairobi.
Togo haina pointi yoyote kufuatia
kupigwa 2-1 na Guinea mjini Casablanca na 3-2 kutoka kwa Ghana katika uwanja
wao wa nyumbani.
Mechi dhidi ya Uganda ndio itatoa
picha halisi ya nani ana nafasi kubwa ya kufuzu katika mashindano hayo
yakayofanyika nchini Morocoo.
0 comments:
Post a Comment