Sunday, September 28, 2014

 
Saimon Msuva ameifungia Yanga goli la ushindi

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WANAJANGWANI, Dar Young Africans wameitandika 2-1 Tanzania Prisons katika mechi ya raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Mabao ya Yanga chini ya kocha Mbrazil yamefungwa na Andrey Coutinho katika dakika ya 34 na la pili likatiwa kambani na Saimon Msuva katika dakika ya 69.

Prisons walijipatia goli la kufutia machozi katika dakika ya 67 kupitia kwa Ibrahim Isaka Hassan.

UCHAMBUZI WA MECHI

Coutinho alifunga goli hilo kwa mpira wa adhabu ndogo takribani mita 24. Haruna Niyonzima aliwadanganya mabeki wa Prisons kama anataka kupiga mpira, lakini akamuachia Coutinho aliyepiga shuti, mpira ukadunda karibu na goli, kipa Mohamed Yusuph akaugusa wakati anajaribu kuokoa, lakini ukazama ndama ya nyavu.


Dakika ya 38 Beki wa Prisons, Jacob Mwalobo aliyekuwa na kadi ya kwanza ya njano alioneshwa ya pili na kuzawadiwa nyekundu na mwamuzi Andrew Shamba kufuatia kumfanyia madhambi Mrisho Ngassa.

Nidhamu mbovu ya ulinzi kwa mabeki wa Prisons ilisababisha wakafunwga goli hilo. Wakati wameweka ukuta waliacha uwazi na nyuma yao alisimama Jaja. Coutinho alipiga mpira ukapita katika eneo hilo na kutikisa nyavu.

Kwa ujumla kipindi cha kwanza, Yanga walitawala zaidi mpira hususani safu ya kiungo.

Mbuyu Twite akicheza nafasi ya kiungo wa ulinzi alishirikiana vizuri na Haruna Niyonzima aliyecheza mbele yake.

Mrisha Ngassa aliyeshambulia kutoka kushoto alikuwa anabadilika na kucheza winga ya kulia na wakati fulani kuingia katikati. Hassan Dilunga aliyeanza winga ya kulia aligongeana vizuri na Niyonzima na mara kadhaa alimuacha beki wake wa kulia Juma Abdul apande juu kuongeza kasi ya mashambulizi.

Coutinho alicheza vizuri nafasi ya kiungo mshambuliaji, ingawa kuna wakati alikuwa anapiga pasi mkaa. Jaja kama kawaida yake hakuonekana sana, kuna baadhi ya mipira alipata na kujaribu kupiga kichwa, lakini hakufanikiwa kufunga goli.

Edward Charles aliyechukua nafasi ya Oscar Joshua aliyeumia mechi iliyopita  hakuwa na presha kubwa kwa upande wake, hivyo alipanda zaidi kuongeza mashambulizi kutoka winga ya kulia.

Hata Juma Abdul naye alipanda zaidi upande wa kulia kuongeza kasi ya mashambulizi.

Prisons walicheza vizuri, mara kadhaa walipiga pasi fupifupi, lakini walikosa kasi ya kwenda mbele. Walijikuta wakikaa zaidi katika eneo lao na kuwapa nafasi Yanga kucheza zaidi safu ya kiungo.

Wajelajela walionekana kukaa nyuma kwasababu walikuwa wachache. Ngassa alishindwa kufurahia mechi hiyo kwasababu Prisons hawakutaka kutoka katika eneo la pili.

Kipindi cha pili Yanga walianza kwa kasi kama kawaida na kulikalia vilivyo dimba la kati.

Dakika ya 55 Dilunga alikwenda benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Thabit. Dakika ya 57, Marcio Maximo alimtoa Coutinho na nafasi yake kuchukuliwa na Saimon Msuva.

Kuingia kwa Msuva kuliongeza kasi zaidi ya Yanga. Dakika ya 61 alitengenezewa pasi nzuri na Niyonzima na kuachia shuti kali ambalo halikulenga lango.


Licha ya kuwa pungufu, Prisons walijitahidi kutengeneza nafasi, lakini walikosa mshambuliaji wa kati.  Julius Kwanga alipata nafasi kadhaa, lakini mashuti yake hayakulenga lango.

Dakika ya 67, Ibrahim Isaka Hassan alifunga goli safi la kichwa akiunganisha krosi iliyochongwa kutoka winga ya kulia na kuisawazishia Prisons.

Ibrahim aliruka juu, Yondani na Cannavaro walimuacha huru kabisa na kipa Dida akajaribu kuokoa mpira huo , lakini hakuwa na la kufanya.

Kuingia kwa goli hilo, kuliwaamusha Prisons na kuanza kupanda juu, lakini nidhamu ya ulinzi haikuwa nzuri.

Dakika ya 69 Saimon Msuva alifunga goli la pili kwa kichwa akimalizia krosi ya Ngassa iliyochongwa kutoka winga ya kulia.

Ngassa kama kawaida aliburuza mpira na kuingiza ndani, mabeki wa Prisons, Jumanne Elifadhili na Lugano Mwangama walishindwa kumzuia Msuva.

Licha ya kufunga, Msuva aliongeza kasi ya Yanga tofauti na mwanzo na hii ilidhihirisha kuwa Maximo hakukosea kufanya mabadiliko hayo.

Dakika ya 81 Ngassa alipata nafasi ya wazi baada ya Mwangama kufanya makosa, lakini alipiga shuti lililotoka sentimita chache kutoka langoni.

Licha ya kuwa pungufu,  dakika za lala salama, Prisons walishambulia lango la Yanga, lakini walishindwa kuwa na mipango ya kupata goli.

Mabeki wa Yanga walilazimika kupigana kufa na kupona kuokoa jahazi na mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa 2-1

Kwa ujumla kipindi cha pili, Prisons ilikuja juu na kupiga pasi nzuri. Walionekana kuwa na kasi na kuipandisha timu juu.

Kikubwa walikosa nidhamu ya mchezo, baada ya kusawazisha goli walikubali kupanda zaidi wakati wako pungufu. Ngassa alikimbizana na beki asiyekuwa na kasi na wakafungwa aina ya goli lilelile waliloifunga Yanga.

Prisons si timu ya kuichukulia poa. Ina upinzani wa hali ya juu na timu nyingine zijipange sana.




0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video