Sunday, September 14, 2014


Afisa habari wa Yanga sc, Baraka Kizuguto (wa kwanza kushoto) Jaja (katikati) na Mbuyu Twite (kulia)baada ya kushinda 3-0 dhidi ya Azam fc jioni ya leo

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

YALE maneno ya ‘Jaja mzito Jaja mzito’ yalizimika ghafla uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Yanga ikichanua kwa mabao 3-0 dhidi ya Azam fc katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliomalizika jioni hii  kuashiria kupenuliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza septemba 20 mwaka huu.

Kama kawaida Jaja na uzito wake alianza mdogo –mdogo katika kipindi cha kwanza na kuonekana kutokuwa na uwezo mzuri, lakini timu zilipoenda mapumziko kwa suluhu ya bila kufungana, kocha wa Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo alimuelekeza nini cha kufanya.

Dakika ya 58’ kipindi cha pili, Jaja aliitendea haki pasi ya winga mwenye kasi kubwa, Saimon Msuva na kuutia mpira nyavuni na kuiandikia Yanga bao la kuongoza.

Mashabiki wa Yanga walilipuka kwa shangwe, nderemo na vifijo kutokana na bao hilo la Jaja na kusahau kuwa ndiye yule  baadhi yao walikuwa wanamlalamikia.

Wakati mashabiki wakiwa na furaha kubwa, Jaja aliandika bao lingine katika dakika ya 66 ya kipindi hicho na kugeuka mfalme akishangiliwa kwa nguvu zote.

Baada ya kumaliza kazi yake aliyotumwa na Maximo, dakika ya 79, aliitwa benchi  na nafasi yake ikachukuliwa na Hussein Javu.

Katika dakika hiyo hiyo, Haruna Niyonzima alitolewa na nafasi yake ikachukuliwa na Mganda Hamis  Friday Kiiza.

Dakika ya 88 kipidi hicho cha pili, Saimon Msuva aliandika bao la tatu na kuzamisha kabisa ndoto za Azam fc kutwaa kikombe cha Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza.

Baada ya kuingia kwa bao hilo, wachezaji wa Azam walionekana kutoamini na kulowa kabisa.

Hata hivyo mabao mawili waliyofungwa kabla na Jaja yaliwafanya wapunguze matumaini na kushindwa kucheza mpira wao uliozoeleka.

Azam walipigiwa kura nyingi ya kushinda mechi ya leo kutokana na kikosi chao kukaa pamoja kwa muda mrefu, lakini Maximo ambaye hana muda mrefu na Yanga alionekana kuwa na mipango mizuri ya ushindi.

Mwaka jana katika mchezo wa ngao ya jamii, bao pekee la Salum Telela lilitosha kuipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam fc.

Kumalizika kwa mechi hii kunamanisha pazia la ligi kuu soka Tanzania limeshafungulia rasmi .

Siku ya ufunguzi (septemba 20 mwaka huu) Azam wataanza nyumbani Azam Complex dhidi ya Polisi Morogoro, wakati mabingwa wa Ngao ya Jamii, Yanga watakuwa ugenini katika dimba la Jamhuri, Mkoani Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mechi nyingine za siku hiyo itawakutanisha Stand United dhidi ya Ndanda fc katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Mgando JKT watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa CCM Mkwakwani, jijini Tanga.

Ruvu Shooting wataikaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani.

Wagonga nyundo wa Mbeya, Mbeya City wataikaribisha JKT Ruvu ya Fredy Felix Minziro katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.


Septemba 21, Wekundu wa Msimbazi Simba chini ya kocha Patrick Phiri wataikaribisha Coastal Union katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video