
Wachezaji wa Young Africans wakishangilia bao
alilofunga Jaja katika mchezo dhidi ya timu ya Azam kwenye Ngao ya Jamii
MABINGWA mara 24 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara timu ya Young Africans kesho watashuka
dimbani kucheza mchezo wa ufunguzi wa VPL 2014/2015 dhidi ya timu ya wakata
miwa wa Mtibwa Sugar kutoka manungu Turinani, mchezo utakaopigwa kwenye dimba
la Uwnaja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kikosi
cha Young Africans kimewasili salama leo mchana mjini Morogoro kwa Bus la klabu
na kufikia katika Hoteli ya kitalii ya Arc iliyopo eneo la nane nane ambapo
wachezaji wote na benchi la ufundi wapo fit kuelekea kwenye mchezo huo.
Majira ya
saa 10 kamili jioni kikosi cha Young Africans chini ya kocha mkuu Marcio maximo
kimefanya mazoezi katika dimba la Jamhuri ambapo pia baadhi ya washabiki
walijitokeza kwa wingi kushuhudia mazoezi hayo ya watoto wa Jangwani.
Wachezaji
walifanya mazoezi kwa takribani saa moja ambapo mara baada ya mazoezi hayo,
washabiki waliofurika waliomba kumsalimia Jaja kila mmoja kwa mukshika mkono
huku kocha Maximo akisema vijana wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
"Tumejiandaa
kuhakikisha tunapata ushindi, natambua Mtibwa wana kikosi kizuri kilichokaa
pamoja kwa muda mrefu, lakini hicho hakiwezi kuwa kikwazo cha kututzuia kuibuka
na pointi tatu dhidi ya wakata miwa" alisema Maximo.
Aidha
Maximo amewaomba wapenzi, washabiki na wanachama wa timu ya Young Africans
kujitokeza kwa wingi kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia mwanzo mpaka
mwisho wa mchezo.
Viingilio
vya mchezo wa kesho ni Tshs 5,000/=
0 comments:
Post a Comment