Wayne Rooney aliandika ujumbe katika mtandao wa facebook akiwajibu watu wanaozidi kuikosoa Manchester United kufuatia kipigo cha Leicester
WAYNE Rooney amesisitiza bado kuna mwanga kwa Manchester United kufanya vizuri msimu huu, licha ya kiwango chao kubadilika-badilika chini ya kocha Louis van Gaal.
Mshambuliaji Rooney, ambaye aliteuliwa na Mholanzi huyo kuwa nahodha majira ya kiangazi mwaka huu, hakuweza kuiokoa Man United na kipigo kizito kutoka Leicester jumapili iliyopita.
Wakiongoza 3-1, United walijikuta wakifungwa 5-3 na Leicester katika uwanja wa The King Power.
Rooney (katikati) alishindwa kuwavumilia wachezaji wenzake baada ya kipigo hicho
Daley Blind (kushoto) naye alikalipiwa na nahodha wake, Rooney baada ya kufungwa 5-3
Rooney mwenye miaka 28 aliteuliwa na Louis van Gaal kuwa nahodha wa United msimu huu.
United wapo nafasi ya 12 katika msimamo wa EPL baada ya mechi tano na tayari wapo nyuma kwa pointi 8 dhidi ya vinara Chelsea.
Wakitarajia kufuta makosa ya msimu uliopita ambapo walishika namba 7, United walimteua kocha mzoefu Van Gaal na wakasajili nyota wakali wakiwemo Angel Di Maria, Daley Blind, Radamel Falcao, Luke Shaw na Ander Herrera.
Rooney anaamini kuwa timu itakaa sawa na imewaondoa hofu mashabiki wanaoonekana kukosa imani.
0 comments:
Post a Comment