BAADA ya kuinyuka Mbeya City fc mabao 4-1 katika
uwanja wa Sokoine jijni Mbeya mwishoni mwa wiki iliyopita, Vipers FC (zamani
Bunamwaya) inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda, itashuka dimbani kucheza mechi
nyingine ya kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani .
Mechi hiyo itapigwa kesho (septemba 16 mwaka hu) uwanja
wa Taifa, Dar es salaam.
Afisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema
kikosi cha Shooting chini ya kocha Mkenya, Tom Alex Olaba kimejiandaa vizuri,
hivyo mashabiki wa soka wajitokeze kuiona timu mpya yenye makazi yake Mabatini,
Mlandizi, Pwani.
“Kesho katika uwanja wa Taifa tutakuwa na mchezo
maridadi wa kirafiki wa kimataifa. Tutacheza na timu ya Vipers FC ya Uganda
iliyotoka kutoa kipigo cha haja kwa ndugu zetu Mbeya City”.
0 comments:
Post a Comment