Friday, September 12, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

MSAFARA wa watu 25 wa timu ya Vipers Sc (zamani Bunamwaya) inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda unatarajia kutua leo nchini tayari kwa mchezo wa kesho wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Wagonga nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc utakaopigwa uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Dar es salaam.

Msafara huo wenye wachezaji 20 na viongozi 5 utatua uwanja wa Ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam na kuunganisha Ndege mpaka uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe, jijini Mbeya.

Afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten amesema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na kitakuwa kipimo kizuri kwa klabu yao kabla ya kuanza michuano ya ligi kuu.

Ten aliwataka mashabiki wa klabu hiyo Mkoani Mbeya na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao.

Kocha mkuu wa klabu hiyo, Juma Mwambusi alisema kuwa anahitaji mechi ya kimataifa ya kirafiki ili kufanya majumuisho ya maandalizi yake na kupata kikosi cha kwanza atakachotumia katika kampeni za kusaka ubingwa.

Mwambusi alisema viongozi walikuwa wanatafuta timu ya Malawi, lakini ikashindikana na mpaka kufikia jana Vipers ya Uganda ilithibitisha kuja nchini.

Mwambusi anayesaidiwa na Suleiman Jabir alisema kuwa wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri na wanajiandaa kutoa changamoto nyingine msimu ujao.

Msimu uliopita, City walishika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Azam fc waliotwaa ubingwa.


Mbeya City wataanza ligi kuu kwa kuwakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Sokoine Mbeya, septemba 20 mwaka huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video