Michael Carrick (katikati akiwa na Chris Smalling na Ryan Giggs) anaweza kucheza nafasi ya beki wa kati Manchester United
MAJANGA ya safu ya ulinzi ya Manchester United yamemfanya kocha Louis van Gaal afikirie kumtumia kwa dharula Michael Carrick katika nafasi ya beki wa kati.
Carrick ambaye ni kiungo wa kati bado anasubiri kuanza mechi yake ya kwanza chini ya kocha mpya na anaimarika pole pole kutoka kwenye majeruhi ya kifundo cha mguu aliyopata majira ya kiangazi.
Lakini kiungo huyo mwenye miaka 33 ameanza mazoezi uwanja wa Carrington na tayari amefanya mazungumzo na Van Gaal kuhusu uwezekano wa kucheza nafasi ya beki wa kati.
Tyler Blackett (kushoto) na Smalling wote walikuwepo katika kipigo cha 5-3 dhidi ya Leicester jumapili iliyopita
0 comments:
Post a Comment