Fred Minziro ( mbele kulia) akitoka uwanjani kwenye moja ya mechi za ligi kuu uwanja wa Taifa msimu uliopita
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
JKT Ruvu chini ya kocha wa zamani wa Yanga, Fred
Felix Minziro iliambulia kichapo cha 2-0 kutoka kwa Kagera Sugar katika mechi
ya raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyopigwa uwanja wa Azam
Complex, Chamazi, Dar es salaam.
Mabao ya Kagera yalifungwa na Salum Kanoni katika
dakika ya 10 na Rashid Mandawa dakika ya 79.
Huo ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Kagera msimu huu
kufuatia kipigo cha 1-0 dhidi ya Mgambo JKT katika mechi ya ufunguzi uwanja wa
CCM Mkwakwani Tanga.
JKT Ruvu wao wanapoteza mechi ya kwanza nyumbani kufuatia
kutoka 0-0 na Mbeya City ugenini wikiendi ya septemba 20 mwaka huu.
Maafande hao jana hawakucheza vizuri ukilinganisha
na mechi ya kwanza kule Mbeya, hivyo ilikuwa halali kuchapwa na Wakata miwa wa
Kaitaba.
Kocha Minziro alikiri wazi kuwa kikosi chake
hakikufanya kazi nzuri, lakini wana takribani wiki moja ya kujiandaa kabla ya
mechi dhidi ya Yanga.
Minziro alisema: “Kwakweli nimeyapokea kwa
masikitiko makubwa matokeo haya. Hali haikuwa nzuri kwa upande wangu.
Tulipoteza umakini na tuliwapa nafasi rahisi wapinzani wetu na wakapata magoli”
“Tumefanya makosa ya kimchezo, nadhani tutafanyia
kazi kabla ya mechi dhidi ya Young Africans”.
0 comments:
Post a Comment