Friday, September 12, 2014

 
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

MAAFANDE wa Tanzania Prisons wametua Dar es salaam kuendelea na mazoezi ya kujiwinda na mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara utakaopigwa septemba 20 uwanja wa Mabatini mkoani Pwani dhidi ya wenyeji Ruvu Shooting.

Prisons waliotua juzi Dar wamesema wamewahi kuja ili kuzoea hali ya hewa ya maeneo ya Pwani ambayo ni joto tofauti na Mbeya kwenye baridi kali.

Kocha mkuu wa klabu hiyo, David Mwamwaja amesema wakiwa Dar es salaam wanatarajia kucheza mechi kubwa za kirafiki dhidi ya Azam fc pamoja na JKT Ruvu ili kujiweka sawa kabla ya kuanza mikikimikiki ya ligi kuu.

“Hali ye hewa ya kwetu ni tofauti na Pwani,  kwahiyo tumewahi kuja ili tuzoee na itatusaidia kufanya vizuri. Tuna mpango wa kucheza na Azam na JKT Ruvu kabla ya kuanza ligi kuu.” Alisema Mwamwaja.

Kocha huyo aliichukua Prisons mwishoni mwa msimu uliopita kuinusuru kushuka daraja isingekuwa ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya mwisho dhidi ya Ashanti United, uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

Prisons wasingeshinda mechi hiyo wangeshuka daraja, wakati Ashanti chini ya Abdallah Kibadeni walikuwa wanahitaji ushindi ili kuwaacha Wajela jela walikuwa wanalingana nao pointi 25.

Ushindi wa Prisons uliifanya ifikishe pointi 28 na kuziacha Ashanti, JKT Oljoro na Rhino Rangers zikishuka daraja.


Kuelekea msimu ujao, kocha Mwamwaja alisema watafanya biashara mapema ili kuepuka mazingira ya kupambana dakika za mwisho.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video