Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
NAHODHA wa Polisi Morogoro Nicholas Kabipe
amefichua siri ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa raundi ya
pili ya ligi kuu soka Tanzania bara iliopigwa jana uwanja wa Taifa, Dar es
salaam.
Simba walikuwa kwa kwanza kuandika bao la kuongoza
katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza kupitia kwa Emmanuel Okwi, lakini Danny
David Mrwanda aliisawazishia Polisi katika dakika ya 50 kipindi cha pili.
Kabla ya mechi ya jana, Polisi walifungwa 3-1 na
Azam fc katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa wikiendi ya septamba 20 mwaka huu
uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Baada ya mechi ya jana dhidi ya Simba, Kabipe
alisema: “Kwa matokeo haya sisi tumefurahi kwasababu tulipoteza mchezo wa
kwanza. Kuna makosa yalikuwa yanatugharimu na Azam wakatufunga magoli matatu.
“Tumerekebisha hayo makosa na tumeweza kupata
sare. Wakati wa mapumziko tukiwa nyuma kwa goli moja kwa bila, mwalimu
alituelekeza kuwa Simba wana kasi sana sehemu ya kiungo”.
“Kwahiyo akasema tunatakiwa tuwe wengi katikati
ili tusiwape nafasi ya kucheza, tuwe tunaenda kukaba watu watatu na tulifanya
hivyo, ikawezekana na tukaweza kupata sare hiyo”.
0 comments:
Post a Comment