Kikosi cha Ndanda fc kilichotoka suluhu dhidi ya Simba sc jumamosi iliyopita uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KUCHEZA mechi ya kirafiki dhidi ya Simba wikiendi
iliyopita kumewafanya Ndanda fc wabaini kasoro za kikosi chao kabla ya kuanza
kwa ligi kuu Septemba 20 mwaka huu.
Ndanda fc waliopanda ligi kuu msimu huu wataanza
kampeni zao dhidi ya wageni wenzao wa Stand United katika uwanja wa Kambarage
mjini Shinyanga, septemba 20 mwaka huu.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Denis Kitambi amesema mechi dhidi ya Simba iliyomalizika kwa
suluhu pacha ya bila kufungana (0-0) katika uwanja wa Nagwanda Sijaona jumamosi
iliyopita imewafanya waweze kubaini makosa yao hasusani safu ya ushambuliaji.
“Tulifuraki kupata mechi na timu kubwa yenye
ushindani mkubwa. Kiufundi kuna mambo kadhaa tumeyabaini. Kwanza kabisa
tunashindwa kutumia nafasi ambazo tunatengeneza, kwahiyo inabidi tulifanyie
kazi.”
“Pia kuna matatizo katika uanzishaji wa mpira
kutoka nyuma, nalo tunatakiwa tulifanyie
kazi.”
“Simba ina ufundi mwingi, kwahiyo ilikuwa mechi
muhimu kwasababu watu kama hao tutacheza nao katika ligi. Tutacheza na Simba,
Yanga , Azam ambao kiufundi unatakiwa kujiandaa zaidi kuliko ule ufundi binafsi
wa wachezaji”
“Mimi naamini wachezaji tulionao hatuwezi kuongeza
wa ziada wala kuwapa lawama sana, kwasababu jambo la kupanga mashambulizi
tunaanza kulifanyia kazi wiki hii iliyobaki na tunataka kucheza kitimu na
kupata magoli.”
“Pia nawapa pongezi wachezaji wangu kwasababu
wanaweza kutengeneza nafasi, hii ilionekana katika mchezo na Simba na mechi
nyingine za nyuma, lakini bado tunahitaji kuzitumia hizo nafasi”.
Kuhusu mechi ya ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya
Stand United, Kitambi alisema atapata changamoto kubwa kutokana na mazingira ya
ugenini.
“Mechi hiyo kwa kiasi fulani imelemea upande wa
Stand United kwasababu wapo nyumbani na unajua wote tumepanda daraja, kwahiyo
na sisi wenyewe tunajua hapo ndipo tunaweza kupata pointi na wenyewe wanajua wanaweza kupata pointi kwetu”
“Faida kwao ni kwamba watacheza nyumbani, kwahiyo
mechi hii itakuwa na changamoto kubwa ukizingatia usafiri kutoka huku Mtwara
kwenda Shinyanga na utatuchosha”
0 comments:
Post a Comment