Louis van Gaal aliitisha kikao baada ya kuchapwa na Leicester
LOUIS van Gaal aliitisha kikao na wachezaji wa Manchester United kilichodumu kwa saa moja baada ya kupigwa kipigo kizito jumapili iliyopita dhidi ya Leicester City, Robin van Persie amefichua siri.
Kocha huyo Mholanzi alinuna kweli-kweli baada ya timu yake kufungwa 5-3 katika uwanja wa The King Power wakati ilikuwa inaongoza kwa mabao 3-1.
Hicho kilikuwa kipigo cha pili wa Man United tangu kuanza kwa ligi kuu England msimu huu.
Robin van Persie, aliyeifungia Man United goli la kwanza dhidi ya Leicester alisema Van Gaal aliwagombeza wachezaji.
Van Persie aliwaambia Fox Sports News: "Usingewezekana (kupoteza kwa namna ile), lakini ilitokea. Tunatakiwa kukabiliana nalo".
"Siku iliyofuata tulikuwa katika hali nzuri. Kwa kiasi fulani kulikuwa na ugomvi na kikao kirefu. Kitu kama saa moja na zaidi".
0 comments:
Post a Comment