Aaron Ramsey wa Arsenal akishika mguu wake baada ya kupata majeraha kwenye mechi dhidi ya Tottenham
ARSENE Wenger amethibitisha kuwa Aaron Ramsey, Jack Wilshere na Mikel Arteta hawatacheza mechi ya wiki ijayo, ikimaanisha nyota hao watatu wanaosumbuliwa na majeruhi wataikosa mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray jumatano ijayo.
Pia wachezaji hawa watatu wako hatarini kuikosa mechi ya ligi kuu jumapili ijayo dhidi ya Chelsea baada ya kupata majeruhi katika sare ya 1-1 jana dhidi ya Tottenham Hotspur uwanja wa Emirates.
Wenger alisema: "Sijui watakaa nje ya uwanja wa muda gani, lakini hawatakuwepo wiki ijayo. Nadhani Ramsey ana majeruhi ya nyama za paja . Wilshere kifundo cha mguu".
Aaron Ramsey akiwa amelala chini kusikilizia maamivu
Jack Wilshere aliumia jana
0 comments:
Post a Comment